Latest Updates

Sauti ya rapper Chid Benz kwenye U Heard ya leo February 26…




Kwenye story ya U Heard ishu ni hukumu ya kesi ya rapper Chid Benz ambayo ilikuwa leo, Mahakama ilitoa hukumu kwamba rapper huyo apewe adhabu ya kifungo au alipe fidia.

Chid amelipa faini ya laki 9 na kuachiwa huru ambapo amesema kuwa kesi hiyo imekuwa ni funzo kupitia maisha ambayo ameishi wakati akiwa kwenye kesi hiyo.

Ni watu wawili waliokuwa karibu na Chid wakati wote wa kesi hiyo, mama yake mzazi ambaye ndiye amelipa faini hiyo pamoja na rafiki yake ambaye hakumtaja.

Akiwa anaongea na Soudy Brown, Chid amewapa pole familia ya marehemu Mzee Ebby Sykes pamoja na Mez B kwa kuwa alikuwa mbali na kushindwa kuhudhuria misiba yote miwili.