Cristiano Ronaldo ameendelea kuudhihirishia ulimwengu kwamba yeye bado ni bora zaidi ya wenzake baada ya kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwa wanasoka wenye utajiri mkubwa kupitia mtandao wa goal.com.
Kwa mujibu wa mtandao huo Ronaldo ana utajiri wa pauni milioni 210 akimuacha nyuma mpinzani wake anayeshikilia nafasi ya pili Lionel Messi mwemye utajiri wa pauni 200.
Utajiri wa Ronaldo si tu unapatikana uwanjani bali pia amekuwa akipata dili la kuwa balozi wa kampuni mbalimbali kama Toyota, Sumsung, Nike na Herbalife ambazo zimekuwa zikifanya naye kazi ya kuzitangaza mara kwa mara.
1. Cristiano Ronaldo
Anatokea Real Madrid: Huyu ndiye mchezaji bora wa dunia na ameendelea kushikilia rekodi yake ya nafasi ya kwanza, ana utajiri wa Euro milioni 210
2. Lionel Messi
Ni mchezaji wa Barcelona: ana utajiri wa Euro milioni 200
3.Neymar Da Silva Santos Jr
Anatokea klabu ya Barcelona: Ni Raia wa Brazil ana utajiri wa Euro milioni 135
4. Zlatan Ibrahimovic
Anatokea klabu ya Paris Saint- German Fc: Ana utajiri wa Euro milioni 105
5.Wyne Rooney
Ni mshambuliaji wa Manchester United: Ana utajiri wa Euro milioni 103
6.Ricardo Kaka
Ni kiungo wa timu ya Taifa ya Brazil na Orlando City: Ana utajiri wa Euro milioni 96
7. Samuel Etoo
Anatokea klabu ya U.C Sampdoria: Ana utajiri wa Euro milioni 87
Raul Gonzalez
Mshambuliaji wa timu ya Al Sadd SC: Ana utajiri wa Euro 85
9. Ronaldinho (Gaucho)
Ni kiungo wa Queretaro F.C: Ana utajiri wa Euro milioni 83
10.Frank Lampard
Ni kiungo wa Manchester City: Ana utajiri wa Euro milioni 80